aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 7, 2013

Tottenham yatoa picha ya Bale kwenye akaunti yao ya Twitter.



Tetesi za kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs 
kuwa mbioni kujiunga na klabu 
ya Real Madrid zimezidi kushika kasi baada ya klabu hiyo kushusha picha ya kiungo huyo
 kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa twitter.
Ukurasa wa Twitter wa klabu ya Tottenham ulikuwa na picha kubwa za wachezaji Gareth
 Bale na Clinton Dempsey lakini picha hizo zilitolewa baada ya Dempsey kujiunga na
 timu ya Seattle Sounders ya Marekani.
Taswira ya ukurasa wa twitter wa klabu ya Tottenham Hotspurs kama inavyoonekana kabla na baada ya kuondolewa kwa picha ya Bale.
Taswira ya ukurasa wa twitter wa klabu ya Tottenham Hotspurs kama inavyoonekana kabla na baada ya kuondolewa kwa picha ya Bale.
Kuondolewa kwa picha ya Bale ndio kumezua gumzo kubwa kwani inaonyesha 
kuwa tayari Spurs wameanza kuchukua hatua za kusonga mbele na kuanza maisha 
bila ya nyota huyo ambaye kwa kiasi kikubwa ametokea kuwa alama ya klabu hiyo.
Wiki iliyopita nyota huyo wa kimataifa wa Wales aliwaaga wachezaji wenzie kwenye
 kikosi cha Spurs   Saa chache kabla ya wachezaji hao kuondoka kwenda nchini 
Ufaransa ambako walikuwa wanacheza mechi ya Kirafiki dhidi ya Monaco .
Real Madrid na Tottenham zimekuwa kwenye mazungumzo juu ya usajili wa
 Bale na mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu kutokana na msimamo wa
 klabu hiyo ya London wa kutaka fedha yote huku Madrid wakitaka kulipa kwa
 awamu .
Pamoja na mazungumzo hayo kuchukua muda mrefu Madrid wanatarajia 
kumthibitisha Bale kama mchezaji wao siku yoyote kabla ya kumalizika kwa kipindi 
cha usajili wakati wa majira ya joto.

No comments:

Post a Comment