aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 11, 2013

TAJIRI ADAIWA KUFUNGA BARABARA ENEO LA KINYEREZI, BONYOKWA ’B’ JIJINI DAR..


 Barabara inayolalamikiwa kufungwa na tajiri ambayo hutumika kwa magari na watembea kwa miguu eneo la la Kinyerezi, Bonyokwa 'B' jijini Dar es Salaam.



                   Ujenzi ulioziba barabara hiyo ukiendelea. 
"Wenye pesa noma" kauli hii inatokana na nguvu walizonazo wenye pesa kiasi kwamba kila jambo wanaloweza kuamua wanaweza kulitimiza na hii ni baada ya tukio la tajiri mmoja anayelalamikiwa na wakazi wa eneo la Kinyerezi, Bonyokwa 'B' jijini Dar es Salaam kwa kutumia fedha zake kufunga barabaya ya eneo hilo. Tajiri huyo ambaye hakutajwa jina lake amefunga barabara kwa ujenzi wa jengo lake unaoendelea eneo hilo. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo malalamiko yao tayari wameyafikisha katika uongozi husika na kwa sasa wanasubiri kuona hatua zipi zitachukuliwa dhidi ya tajiri huyo.


No comments:

Post a Comment