aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

MOYES: "SIHITAJI KUMSHAWISHI WAYNE ROONEY AU MCHEZAJI YEYOTE KUICHEZEA MANCHESTER UNITED"


Huku tetesi mpya zikizuka kila siku juu ya 
hatma ya mshambuliaji  Wayne Rooney, 
kocha wa Manchester United David Moyes 
amesema jana Jumanne kwamba hahitaji 
kumshawishi mshambuliaji aendelee kubaki 
Old Trafford.
Alipoulizwa kuhusu namna Wayne Rooney 

alivyolipokea suala la United kukataa ofa 
mpya ya Chelsea ya £30m kwa ajili kumsajili,
 Moyes alisema, "Sijui, sijamuuliza kuhusu 
suala hilo."

Pia wakati akijibu swali la kama atamshawishi 

nyota huyo wa England aendelee kubaki kuitumikia 
klabu hiyo inayojinadaa kutetea ubingwa wake wa
 EPL, Moyes alisema: "Huhitaji kumshawishi mtu 
yoyote kuichezea Manchester United."
Moyes alikuwa akiongea na waandishi wa habari 

baada ya mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya 1-1 
dhidi ya AIK jijii Stockholm.

No comments:

Post a Comment