aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

MOTO WAUA WAWILI DAR,MMOJA AJINYONGA...


WATU watatu wamekufa katika matukio mawili tofauti jijini Dar es Salaam, wakiwemo wawili walioteketea kwa moto baada ya nyumba kuungua, huku mwingine ambaye ni msichana wa miaka 16 akifa kwa kujinyonga. Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi, aliyejinyonga ni Milika Kusenha.
Alisema binti huyo alikutwa akiwa amejinyonga juzi saa 1:00 asubuhi maeneo ya Vingunguti Mtakuja, wilaya ya Ilala.
Alijinyonga kwa kutumia kitenge na mtandio alivyoviunganisha na kufunga kwenye kenchi chumbani kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina la Naomi Milimo (24), aliyekuwa anaishi nae. Hata hivyo sababu za kujinyonga hazijafahamika, maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika tukio jingine, moto uliozuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na Ramadhani Kambenga yenye vyumba vinne, uliteketeza kabisa vyumba hivyo pamoja na kusababisha vifo vya watu wawili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema moto huo ulizuka juzi saa 5:00 usiku katika eneo la Keko Mwanga na vyumba viwili vya mpangaji aitwaye Michael David (28) pamoja na mali zote, pia kumuunguza mtoto wake aitwaye Johnson Michael (6) na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Abuu anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 35.
Kutokana na miundombinu mibovu ya barabara magari ya zimamoto yalishindwa kufika katika eneo la tukio, moto huo ulizimwa na wananchi wa eneo hilo kwa kutumia mchanga na maji. Chanzo cha moto huo inasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Maiti zimehifadhiwa hospitali ya Temeke, upelelezi unaendelea. Katika tukio la tatu, moto ulizuka ghafla katika nyumba ya Komba Dominick (68) mkazi wa Mtoni Mtongani na kuteketeza mali zenye thamani ya Sh milioni 26.
Kamanda Kiondo alisema tukio la moto huo lilitokea juzi saa 7:00 mchana Mtoni Mtongani, ambapo uliteketeza ghala la kuhifadhia makasha matupu mali ya mpangaji Lameck Anania (55).
Pia moto huo ulishika nyumba ya jirani aitwaye Mahamudu Chibango (53) na kuunguza nyaya za umeme pamoja na vyumba viwili.
Moto ulizimwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji cha jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

No comments:

Post a Comment