aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 7, 2013

MGANGA AUWAWA KIKATILI....!!

 
MGANGA wa jadi, George Tereva (55) mkazi wa Kijiji cha
 
 Lungemba wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa ameuawa kikatili 
 
baada ya watu wasiojulikana kwenda nyumbani
 
 kwake na kupiga risasi tatu katika maeneo
 
 
ya tumboni, kichwani na kwenye paji lake la uso.Pia watuhumiwa
 
 hao walimcharanga mganga huyo kwa panga kichwani na
 
 kutoweka bila kuchukua mali zozote za

 marehemu huyo
 
.Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi alisema tukio hilo la kusikitisha lilitokea Augosti 4, mwaka huu, saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Lugemba.Kamanda huyo alisema, tukio hilo lilitokea baada ya watu wawili wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kuanza kumfyatulia risasi hadi kuuondoa uhai wake ambapo pamoja na kumuua kwa risasi waliendelea kumcharanga kwa panga.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi Mkoa wa Iringa, Dkt.
 
 Galus Msekwa akizungumzia tukio la kuuawa kwa mganga
 
 mwenzao, George Tevere ambaye alikuwa
 
 anawatibu wagonjwa kimeisikitisha jumuiya yao mkoani humo. 
 
 
"Watu walikwenda kwa mganga huyo kuomba gari kwa malengo ya
 
 kutaka wasafirishiwe mgonjwa wao hadi anapoishi mganga huyo, 
 
lakini alipotoka ndani ya nyumba ili awasikilize ndipo walipoanza
 
 kumshambulia kwa kumpiga risasi tumboni;"Kichwani na baadaye kuanza kumcharanga kwa mapanga katika maeneo ya mwili wake hasa kichwani hadi kusababisha kifo chake, suala hili limetushtua sana," alisema Dkt. Msekwa.


No comments:

Post a Comment