aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

KUTANA NA MASTAA… UCHUMBA 100%, NDOA 0%

...WALIANZA UHUSIANO WA KIMAPENZI TANGU MWAKA 2000 WAKATI HUO ISABELA AKIWA KIDATO CHA PILI HIVYO KUUFANYA...
NDOA ni matokeo mazuri ya uchumba. Ili mtu ufikie kwenye ndoa lazima upitie katika hatua ya uchumba lakini kwenye uchumba huo, watu hutofautiana.
Rose Ndauka akiwa na mchumba wake Maliki Bandawe.
Wapo wanaoudumu kwa muda mrefu bila ndoa lakini wapo ambao hawachukui hata mwaka kwenye uchumba, wanaoana.
Ukilinganisha wale wanaodumu kwa mwaka mmoja wa uchumba, wale wa zaidi ya miaka mitatu watakuwa wanaleta tafsiri rahisi kwamba uchumba wao umeshiba asilimia mia moja lakini wanakuwa hawaamui kuoana.
Leo katika makala haya tunawachambua baadhi ya mastaa ambao wamedumu kwa zaidi ya miaka mitatu bila ndoa, baadhi yao wamefikia hadi hatua ya kuzaa kabla ya ndoa.

ROSE NDAUKA & MALIKI BANDAWE
Rose ni msanii wa filamu Bongo. Wawili hawa ni wachumba wa muda mrefu, zaidi ya miaka mitatu tangu walipoanza kusema watafunga ndoa. Hadi sasa hakuna ndoa, wanaogelea katika uhusiano wa kimapenzi kwa kuishi pamoja.

RACHEL HAULE ‘RECHO’ &   GEORGE SAGUDA
Msanii huyu wa filamu za Kibongo na mchumba wake ambaye huwa anakaa nyuma ya kamera kama muongozaji huku akiwa anapiga mzigo TRA, wamedumu kwenye uhusiano kwa miaka mitano ambapo kwa mujibu wa Recho hakuna hata mpango wa ndoa, bado sana.
Wawili hao wanaishi pamoja kama mke na mume.
SHAMSA FORD & DICKSON
Wawili hawa wamedumu kwenye uchumba kwa takriban miaka minne sasa. Katika uchumba wao wamejaliwa kupata mtoto mmoja. Hivi karibuni Shamsa alitangaza kuwa lazima wafunge ndoa ndani ya mwaka huu lakini kabla ya hapo, alikuwa amekataa katakata suala la ndoa.
ISABELA MPANDA & LUTENI KALAMA
Isabela ni msanii wa filamu na muziki pia, aliwahi kushikilia Taji la Miss Ruvuma. Kalama ni msanii wa muziki wa kizazi kipya. Wawili hawa wanaongoza kwa kudumu, walianza uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2000 wakati huo Isabela akiwa kidato cha pili hivyo kuufanya uhusiano wao udumu kwa takriban miaka 13.
Pamoja na kukaa katika uhusiano kwa miaka yote hiyo, suala la ndoa bado halijulikani kwani kila mara wamekuwa wakitangaza kuoana lakini ahadi haitimii.
ELIAS BARNABA ‘BARNABA’ & ZUBEDA
Barnaba ni mwanamuziki wa Bongo Fleva yeye na Zubeda (Mama Steve) ni mtu na mzazi mwenzake kwani wamejaliwa kupata mtoto mmoja, Steve.
Wawili hawa wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne sasa lakini suala la ndoa hawajawahi kulizungumzia, wapenzi hawa waliunganishwa na msanii wa filamu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ikiwa ni baada ya Barnaba kumkuta Zubeda nyumbani kwa Aunty Lulu.

EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’ & SIWEMA
Nay wa Mitego ni msanii wa Bongo Fleva. Msanii huyo amedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi na mchumba wake Siwema kwa zaidi ya miaka mitatu.
Hivi karibuni wawili hawa walipatwa na tatizo baada ya ujauzito aliokuwa nao Siwema kutoka, suala la kufunga ndoa bado halieleweki.
HERRY SAMIR ‘MR BLUE’ & WAHIDA
Mr Blue staa wa Bongo Fleva na Wahida ni wapenzi wa muda mrefu na uhusiano wao kwenye vyombo vya habari una zaidi ya miaka miwili, imedaiwa kabla ya hapo pia walishakaa miaka kadhaa.
Wawili hao wamejaliwa kuwa na mtoto mmoja lakini mpaka sasa hawajatoa muafaka wa kufunga ndoa.

No comments:

Post a Comment