aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 9, 2013

JB, "NAPENDA SANA KULA KULA VYAKULA..."



JB bonge la bwana mwigizaji wa filamu Swahiliwood

MWIGIZAJI mahiri wa filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ amedai kuwa mwili wake umekuwa gumzo hata mwenyewe anakereka kwa kuongelewa kama bonge hata watu kuhisi kama labda unampata shida katika kutembea au ni mtu asiye na mazoezi kumbe yeye ni mwepesi kama Messi mchezaji wa mpira wa Barcelona fc ambaye anaweza kupenya ngome yoyote ya wapinzani. 

Jacob stephenJB Bonge la Bwana akiwa na mwigizaji Stara.

Jacob stephen
“Ni kweli kuna wakati nahitaji kufanya mazoezi lakini tatizo si mazoezi kwangu unene huu ni kwa sababu moja tu kula sana chakula kingi kila wakati nakula sana nahisi hata Oxfam hawakukosea kunipa ubalozi wa chakula ni sehemu ambayo nastaili napenda sana kula kula vyakula na ndio huu unene unao uona sasa,”anasema JB. 
JB mwigizaji bora anayetamba na filamu zinazotikisa kwa sasa za Nakwenda kwa Mwanangu na Zawadi yangu, anasema kuna wakati unene unamtesa sana na kutamani apungue kwani unene huo unamtesa hasa katika mavazi, kwa sababu mavazi anayovaa kwa sasa anaagiza kutoka nje ya Nchi baada ya kutuma vipimo hivyo kama anahitaji nguo haraka ni vigumu kufika kwa wakati hiyo inatokana na kukosa mafundi au wabunifu wa hapa nchini. 

No comments:

Post a Comment