aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 12, 2013

HUYU NDO MBUNGE SHAROBARO WA KENYA AITWAYE SONKO ALIVYOHUDHURIA KATIKA SHOW YA DIAMOND KENYA

Tarehe 9.8.2013 nilikuwa nchini Kenya kikazi zaidi nikimaanisha
kuwajibika stejini,kukonga nyoyo za mashabiki
wa Nairobi ambao kwa mara ya kwanza nilikuwa nafika jijini 

hapa kikazi..!!
Namshukuru Mungu kila jambo lilienda sawa na kushuudia
 umati wa maelfu ya wakenya wakifurahia
kile walichokuwa wakikiona toka kwangu na team yangu nzima
ya wasafi,Lakini tusicheze mbali sana
hapa nipo kukujuza zaidi jambo ambalo nililiweka kama
 kiporo nije kukupa siku ya Leo.
Nilipowasili 'KICC' moja kwa moja nilienda nyuma ya
 jukwaa,Ebhana eeeeh sikuamini niliokutana nao
kiukweli niliamini hata wasanii wenzangu kutoka nchi za
ukanda wa Afrika mashariki wanakubali
kazi zangu na wanafurahia muziki wangu kiujumla.....
Alikuwepo Seneta wa wakenya.Seneta wanatumia jina ilo nchini kenya lakini
naweza muita Mbunge wa Jiji la Nairobi
Anaefahamika kama Mike Sonko,Mbunge kijana zaidi
kwenye bunge la kenya ,ukifika jijini
Nairobi na ukataja jina lake basi lazima wananchi wa
eneo lile wajue ni mmoja wao.....
Seneta huyu alikuwepo kwenye show hii sambamba
akiwa na Mkewe pamoja na
watoto wake wawili,Muda ulivozidi kwenda kabla ya
Show kuanza pia alikuwepo
Msanii anaefanya vizuri kwa sasa afrika
mashariki,hapa namzungumzia,
Jaguar anetamba na kibao cha Kigeugeu alikuwepo kushow love kwenye show yangu
kikamilifu zaidi maana niliwakuta basi ina maana walifika muda eneo lile ambalo
linachukua zaidi ya watu 3,000 na kwa siku hiyo kwa mujibu wa http://www.ghafla.co.ke kutoka
Nairobi wanasema apakuwa na sehemu iliyobakia wazi hadi waliamuru geti kufungwa
kuepusha kutokea chochote na kuimarisha usalam...!! Seneta Sonko ndie alikuwa
Msema chochote yani 'MC' kipindi ulipofika
muda wa kupanda jukwanii .alinikaribisha stejini
kwa mbwembwe,zile shangwe toka kwa watu wa nairobi zilizidi kunipa
mizuka ya kufanya unyama wangu hatari kabisa kuakikisha
naacha alama jijini hapa...
Pia kundi zima linalofanya vizuri kwa afrika mashariki na kati walikuwepo
hapa nawazungumzia Sauti Soul kutoka Nairobi walikuwepo wakishow love
siku hiii,Hii ilinipa moyo sana na kuendelea kumshukuru Mungu kwa
mkono wake wa baraka ulioshukia kwangu hadi kufika hapa nilipo
kupata kibari kila ntakapotia mguu.....
Kama ulikuwa ujui Mbunge huyu licha ya kuwa na cheo hiko
anapenda sana  muziki na kutoa
msaada sana kwa chipukizi nchi kenya,kabla ya show alionekana
 mwenye furaha nyuma ya jukwaa
alionekana yeye na watoto wake wakicheza muziki uliokuwa unalia kwa sauti ya chini
baada ya kuvuta hisia nikagundua ni Kulewa ilikuwa inatwangwa muda huo,
Napenda kushukuru kila mmoja aliekuwepo usiku ule na kushow love pamoja nami,
Hakika Mungu atawabariki zaidi na zaidi.....
Appearance:Senator,Mike Sonko
                    Jaguar
                    Sauti Soul

No comments:

Post a Comment