aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 9, 2013

Hizi ndo mbinu za kuishi na mpenzi wako na kudumisha mahusiano yenu mhimu kujua

Hata kama utapinga haya, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo

wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.

Jinsia zote zina umuhimu na jambo hili muhimu, lakini kuna tofauti kidogo, kwamba mwanamke

anasubiri kufuatwa na mwanaume, wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake. Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.

Wanawake wa ‘mjini’ huwa hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume. Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hisia tofauti na kila mwanaume.

Tuyaache hayo, hoja kubwa ya msingi hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.

Katika matoleo yaliyopita, niliwahi kuzungumza kuhusu namna gani mwanamke anaweza kuwashawishi wanaume wakataka kuingia katika uhusiano naye. Leo nazungumzia juu ya wewe ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa unaitaka. Unajua cha kufanya? Fuatana nami.

EPUKA MAKUNDI HATARI

Mwanaume anapenda kuwa na mke mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.

Lakini yawezekana, jamaa alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa mbali na makundi ya wanawake hatari! Umenipata?

ZINGATIA MAVAZI YAKO

Kila mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu anapenda nini na nini anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo. Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!

Huzuiwi, lakini swali la msingi, mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim anaona sehemu zako za faragha hadharani?

Ukiachana na chaguo la mwenzi wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue! Jisitiri vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili wako ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.

JIPE MOYO

Hili nilishawahi kulizungumza sana katika mada zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya kuolewa au watahangaika sana lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!

Mwingine anajinyima mwenyewe nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”

Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.

Unaitengeneza kwa misingi ya kwanza, kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo baadaye.

Iko hivi, ukianza kujishusha mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani moyoni, hapo sasa ni mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa mtindo huo.

ACHA PAPARA

Haizuiwi kuuliza kuhusu mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi. Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia kumfanya jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake yanaweza kumpa picha tofauti.

Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu...”


Dada yangu, acha hizo, utampoteza!

No comments:

Post a Comment