aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

CRISTIANO RONALDO AITUNGUA CHELSEA MABAO MAWILI NA KUMWAMBIA MOURINHO - "NAPENDELEA KUZUNGUMZA KUPITIA MATENDO YANGU YA UWANJANI"

Cristiano Ronaldo alikuwa na sababu nyingi zaidi ya kushangilia 
goli lake katika mechi ya pre-season - na kumuonyesha boss wa 
Chelsea Jose Mourinho aliyemdhiaki kabla ya mchezo kwamba 
yeye ni "Ronaldo" wa aina gani.

Ronaldo alifunga mabao mawili na kuiwezesha Real Madrid 
kuifunga 3-1 Chelsea katika Guinness International Champions 
Cup jijini Miami.

Baada ya goli lake la kwanza alilofunga kwa mkwaju wa faulo,
 hakushangilia bali aligeuka mbele ya jukwaa la mashabiki na 
kuonyesha kifua chake huku akitikisa kichwa.
 Baada ya mchezo huo Ronaldo alizungumza na waandishi wa 
habari kuhusiana na maneno ya maneno Mourinho kwamba 
Ronaldo orijino ni yule wa Brazil - Cristiano alisema: 
"Napendelea kuzungumza kwa vitendo vyangu vya uwanjani 
na sio mara pengine popote"


No comments:

Post a Comment