aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

COASTAL UNION YAMSAINISHA MGANDA ALIYEZINYANYASA SIMBA NA YANGA KUTOKA URA




Klabu ya Coastal Union imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa 
kiganda Yayo Lutimba kutoka timu ya mamlaka ya mapato ya
 Uganda URA. 

Aliyefanikisha zoezi hilo ni meneja wa Wagosi, Akida Machai ambaye 
amepanda ndege mpaka jijini Kampala kunasa saini ya kijana mdogo
 mwenye miaka 19, Yayo Lutimba Kato kutoka timu ya mamlaka ya 
mapato Uganda (URA).

Nassor Ahmed ‘Binslum’, ambaye ni mkurugenzi wa ufundi amesimamia 
kwa kiasi kikubwa kufanikisha usajili wa wachezaji takriban tisa 
ukijumlisha na Kato amezungumza na blog hii usiku wa leo baada ya 
Meneja Machai kuenda kumtambulisha Kato kwa Binslum na kuweka 
wazi kuwa tatizo la ukame wa mabao litaisha kwa wana Mangush.

Itakumbukwa kocha Mkuu wa Coastal Union, Hemed Morocco wiki chache 
zilizopita wakati wa kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA,
 aliweka wazi bado kikosi chake kina matatizo ya umaliziaji.

Alibainisha kikosi hicho kipo vizuri kila idara kuanzia golikipa, mabeki na
 viungo ila hakuna mtu mwenye uchu wa mabao hivyo kuahidi kuwatumia
 wachezaji haohao kuwafundisha namna ya kuadhiri magolikipa wa
 timu pinzani.

Ndiyo maana winga Danny Lyanga alikuwa akichezeshwa namba kumi ili 
kumuangalia uwezo wake wa kupachika mabao lakini hakuonekana kucheza 
vema kwenye mechi ya URA.

Kwa usajili wa miaka miwili kuitumikia Coastal Union kinda huyu atakuwa
 na nafasi nzuri sana kujitengenezea jina nchini Tanzania hasa baaada ya
 kuwa na rekodi nzuri ya kuwafunga Simba na Yanga mabao mawili 
mawili katika mechi walizokutana nazo kwa vipindi tofauti.

Zipo taarifa kuwa Yanga nao walikuwa mbioni kumnyakua kinda 
huyu lakini Meneja Akida Machai amewazidi akili kwa kumfuata 
hukohuko kwao Uganda. Na hizi ni mbinu za ‘kimafia’ zinazotumiwa 
na timu kubwa duniani kote kunasa wachezaji mahiri.

Mungu akipenda kesho Kato ataungana na wachezaji wenzake 
katika kambi iliyopo pembezoni mwa bahari ya hindi Raskazone 
Hotel, jijini Tanga.


Wagosi wameanza vizuri mechi zao mbili za majaribio ambapo 
mechi ya kwanza walishinda bao 1-0 dhidi ya URA na siku tatu 
baadaye wakashuka dimbani dhidi ya Simba SC ambao nao 
walichapwa 1-0. Zipo taarifa za kucheza mechi ya kirafiki 
siku ya Eid pili uwanja wa Mkwakwani lakini zikishathibitishwa 
na timu tutakayocheza nayo tutawahabarisha.

No comments:

Post a Comment