aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 12, 2013

CHAKULA CHAUA NDUGU WANNE,13 WENGINE HOI...



WATU wanne wa familia moja wamefariki na wengine 13
 
wamelazwa hospitalini kutokana na kula chakula chenye sumu 

wakati wa sikukuu ya Idi el Fitri.Watu hao wamelazwa
 
Kituo cha Afya cha Lusewa wilayani Namtumbo na Hospitali ya

Serikali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO).


Kamanda wa Polisi Mkoa Deusidebit Nsimeki, alisema tukio hilo
 
lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 7:00. Kamanda Nsimeki,

alisema siku hiyo kabla ya tukio, Salum Mumba, alinunua samaki 

aliyepeleka nyumbani kwa ajili ya sikukuu ya Idi.Kamanda

 Nsimeki alisema katika tukio hilo Polisi wanamshikilia

 mtu mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina ambaye atasaidia polisi

 kwenye upelelezi wake. 
 

Alisema baada ya kula chakula hicho, haikuchukua muda mrefu

 mtoto alianza kuumwa naye baadaye alifariki dunia. Baadaye

watoto wawili walianza kuumwa na kufariki. Watu wengine 13

 walianza kuumwa baadaye majirani walipata taarifa kuwakimbiza

 watu hao hospitali. 
 

Aliwataja waliolazwa katika kituo cha afya cha Lusewa kuwa ni 

Tazamio Mumba, Zidani Mumba, Ramadhani Mumba na Zahara 

Mumba wote wakazi wa kitongoji Tulieni B. 
 

Waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Songea kuwa ni Gairi

Mumba, Zamoni Mumba, Fatuma Rashidi, Samidu Mumba, Asha

 Omary na Sharifa Mumba. 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi ya Hospitali ya Mkoa Songea Dkt. Benedictor Ngaiza alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo hali zao zinaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment