aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

BREAKING NEWS: FABREGAS AIKATAA RASMI MAN UNITED - ASEMA ANAHESHIMU KUMHITAJI KWAO LAKINI ANA FURAHA BARCELONA NA ANGEPENDA KUBAKI.


Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas hatimaye amevunja ukimya
 kuhusu suala la Manchester United kutaka kumsajili kwa kusema 
anataka kubaki nchini Spain. 

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano 
wa waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur mahala ambapo  
Barcelona wapo kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya. 

Fabregas alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea 
Barcelona na hakuna kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa 
hapa na sijawahi kufikiria kuhusu kuondoka. 

"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote 
kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.  

'Ni heshima kubwa kwa Manchester United kuleta ofa mbili kwa 
ajili yangu, lakini hakujawahi kuwa na mazungumzo. Sijawahi 
kuongea na klabu yoyote tangu nimejiunga na Barcelona miaka 
miwili iliyopita.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. 
Kila mut ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata 
ishara yoyote tofauti ya kuhisi sihitajiki. 
'Sikutaka kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi 
kila kitu kilikuwa wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki 
hapa. Niliiambia klabu nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli
 - hasa la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,'
 alisisitiza Cesc Fabregas

No comments:

Post a Comment