aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

BAADA YA SUAREZ: SASA WAYNE ROONEY NAE AONDOLEWA KUFANYA MAZOEZI NA KIKOSI CHA KWANZA CHA UNITED - APELEKWA KIKOSI CHA PILI

Siku moja baada ya Liverpool kumuondoa Luis Suarez kama 
mazoezi ya kikosi cha kwanza na kumlazimisha kufanya mazoezi 
pekee yake, leo hii Wayne Rooney nae amefanyiwa kitendo hicho 
hicho na kocha wake wa Manchester United David Moyes kwa 
kumpeleka mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka kufanya 
mazoezi na kikosi cha pili cha timu ya mabingwa wa England. 

Rooney alikuwa ndio mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza 
kilichokuwa kikifanya mazoezi na wachezaji wa ziada katika 
uwanja wa mazoezi Carrington, in a session chini ya usimamizi 
wa makocha Warren Joyce na Nicky Butt.

Mchezaji huyo anayetakiwa kwa udi na uvumba na Chelsea leo 
alienda mazoezini asubuhi akitegemea kufanya mazoezi na 
wachezaji wenzie wa kikosi cha kwanza lakini akaondolewa na 
Moyes na kupelekwa wanapofanya mazoezi wachezaji wa kikosi 
cha pili.

No comments:

Post a Comment