aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

BAADA YA KUIPAKA LIVERPOOL - LUIS SUAREZ AAMRIWA KUFANYA MAZOEZI PEKE - BRENDAN ROGERS AKANA KUMPA AHADI YA KUONDOKA IKIWA HAWATOKUWA TOP 4


Mshambualiaji wa Liverpool Luis Suarez amepewa amri ya 
kufanya mazoezi peke yake na kocha Brendan Rodgers, 
ambaye amesema hatua hiyo inakuja baada ya mshambuliaji
 huyo kuikosea heshima klabu hiyo. 
Rodgers pia amekataa taarifa alizotoa Suarez kwamba klabu 
ilimhaidi kwamba ikiwa Liverpool watafeli kufuzu kucheza 
Champions League.
Suarez, 26, anajipanga kuwasilisha ombi rasmi la kuuzwa wiki
 hii ikiwa uhamisho wake utazuiwa. 
"Hakujawahi kuwa ahadi yoyote ya namna hiyo baina yetu -
 kwa kifupi ahadi yoyote, na kwa maana hiyo hakuna ahadi 
iliyovunjwa," alisisitiza Rodgers.
"Klabu na wawakilishi wake walikuwa na mazungumoz kadhaa 
na alijua kila kitu kilivyokuwa kinaendelea .
"Ameikosea sana heshima klabu - lakini klabu hii ilimpa na 
kumfanyia kila kitu. 
"Maneno yake niliyoyasoma kwenye vyombo vya habari 
yamenisikitikisha sana - lakini kazi yangu ni kubwa zaidi 
ya hili suala. "
Vyanzo vya karibu na Liverpool vinasisitiza uamuzi wa 
kumlazmisha Suarez afanye mazoezi kimpango wake 
ulifanywa kabla hata mchezaji huyo hajaongea jana na 
vyombo vya habari, hivyo uamuzi huo umetokana na 
kucheza kwake chini ya kiwango kwenye mechi za kirafiki. 
Rodgers aliongeza: "Nitachukua maamuzi magumu juu ya 
suala hili. Nadhani Luis anajua sapoti aliyokuwa akipata 
kwenye klabu hii na hilo limekuwa jambo la siku zote.
"Kazi yangu ni kupigana na kuilinda klabu hii. Mazungumzo 
niliyokuwa nayo na yeye, anajua yalikuwa na yataendelea 
kuwa binafsi kati yangu na yeye."

No comments:

Post a Comment