aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

Arsenal wawanyuka Manchester City

20130810-221519.jpg

Arsenal wawanyuka Manchester City

By Israel Saria on August 10, 2013
Licha ya kutopata nyota wake inaowasaka kuimarisha mashambulizi, Arsenal wamewakata maini Manchester City kwa kuwatandika mabao 3-1.
City wanaofundishwa na kocha mpya, Manuel Pellegrini, wanafikiriwa kuwa na washambuliaji wakali zaidi kwa msimu unaoanza Jumamosi ijayo.
Arsenal walionekana kupewa nguvu ya aina yake na Theo Walcott aliyecheza vyema katika mechi ya kirafiki iliyopigwa nchini Finland.
Washika Bunduki wa London walianza kucheka na nyavu katika dakika ya 24 kwa bao lililofungwa na Walcott aliyemchambua kipa Joe Hart kwa juu, baada ya kupasiwa vyema na Aaron Ramsey aliyemaliza msimu uliopita vyema.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wamemaliza programu yao ya kujiandaa kwa Ligi Kuu kwa ushindi katika mechi tano, sare moja na kufungwa moja, tangu kuanza kwa ziara hizo Julai.
City kwa upande wao wameshinda mechi tatu na kufungwa nne, hitimisho likiwa hiyo ya Jumamosi hii jioni.
Walcott alifunga tena bao la pili baada ya mapumziko, akitengewa pia na Ramsey, kisha akampiga chenga kipa Hart kabla ya kutundika mpira kwenye kamba.
Alikuwa walcott tena aliyesababisha kilio Etihad, lakini safari hii alimpigia pasi mshambuliaji Mfaransa, Olivier Giroud ambaye hakufanya ajizi kujaza mpira golini.
Mshambliaji mpya wa City aliyetoka Sevilla ya Hispania, Alvaro Negredo alifunga bao la kufutia machozi kwa kumzidi maarifa kipa Lukasz Fabianski kwa kupitisha mpira pembeni mwake katika dakika ya 80.
Arsenal wanaanza kipute chao kwa kuwakaribisha Aston Villa Emirates Jumamosi, wakati City watakuwa wenyeji wa Newcastle hapo Etihad Jumatatu inayofuata.
Vikosi vilivyochuana vilikuwa hivi – Arsenal: Szczesny (Fabianski 46); Sagna (Jenkinson 73), Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Arteta (Perez 67), Wilshere (Cazorla 46), Ramsey (Hayden 88); Oxlade-Chamberlain (Zelalem 73), Walcott, Podolski (Giroud 46).
Manchester City: Hart; Zabaleta (Richards 46), Kompany, Lescott (Boyata 85), Clichy; Milner (Jesus Navas 46), Fernandinho (Rodwell 79), Toure (Javi Garcia 67), Silva (Jovetic 67); Dzeko (Nasri 46), Negredo.

No comments:

Post a Comment