aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

AFARIKI BAADA YA KUJERUHIWA NA PANGA...

Ilidaiwa kabla ya hapo, wakati wakicheza, kulitokea ugomvi kati yake na mwenzake aliyekuwa akicheza naye, Nyanswi Magaigwa, baada ya Joseph kuliwa Sh 5,000.
Katika ugomvi huo, inadaiwa Magaigwa alichukua panga na kumjeruhi mwenzake shingoni na kisogoni, ambapo majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya na kupatiwa matibabu kabla ya kurejeshwa nyumbani.
Kamanda Kamugisha alisema Joseph aliendelea kupatiwa matibabu akitoka nyumbani na ilipofika Agosti 4 saa moja asubuhi, alifariki dunia na mwili wake ulipofanyiwa uchunguzi, ilibainika chanzo cha kifo chake ni jeraha alilopata shingoni.
Polisi inamsaka mtuhumiwa na raia wema wameombwa kutoa taarifa mara watakapomwona Nyanswi, ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Wakati huo huo katika kijiji cha Kinesi, kata ya Nyamunga, wilayani Rorya, mtoto Baraka Chacha (4), amechoma nyumba wakati akichezea kiberiti.
Baraka ambaye hakupata majeraha baada ya kuokolewa, alipokuwa akichezea kiberiti, inadaiwa aliwasha moto godoro na kusababisha usambae katika nyumba nzima, mali ya William Mabala.
Kamanda Kamugisha amewatahadhalisha Wazazi kuwazuia Watoto wao kuchezea moto kwani hasara kama hiyo imesababishwa na wazazi kutowakanya watoto wao kuchezea moto.

No comments:

Post a Comment