aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 6, 2013

ACTRESS LUCY KOMBA ASAINISHWA NA KAMPUNI YA TWALEB ENTERTAINMENT NCHINI DENMARK. ..

Lucy Komba
 
Actress maarufu Swahiliwood Lucy Komba amesainishwa mkataba wa kufanya kazi zake za filamu na kampuni ya nchini Denmark inayoitwa Twaleb Entertainment ambayo inamilikiwa na Abou Hermis Twaleb mtanzania anayeishi nchini humo kwa takribani miaka 12 sasa tangu mwaka 2001. Akizungumza exclusively na Swahiliworldplanet juzi Twaleb alisema "kwa kifupi ni kwamba Lucy Komba ameshaingia mkataba na Twaleb Entertainment ambayo mimi ndio mmiliki. Nimefurahi sana kuwa karibu na Lucy na kwa kuwa namkubali sana kikazi katika tasnia ya filamu na hakuna atakayepinga ninachokisema. Na kwa upande mwengine ni mtu muhimu sana tofauti na baadhi ya mastaa wengine kwa kuwa uwezo wake ni mkubwa kiasi cha kunifanya niwe navutiwa sana na uchapaji kazi wake kwa kuwa yeye ni kila kitu nikimaanisha ni actreess, producer, director na pia ni writer mzuri sana wa story . Na ndiyo sababu nimeamuwa kufanya naye kazi ingawa tayari wapo wasanii wengi wengine ambao tayari wameshawasiliana na mimi kuhusu kuja kufanya kazi na mimi katika siku zijazo". Soma zaidi
Kampuni hiyo inaanza kutengeneza filamu yake ya kwanza mwezi huu wa nane huku Lucy Komba akiwa mmoja wa waigizaji wakuu "Utengenezaji wa film yangu ya kwanza unaanza mwezi huu huu baadaye na Lucy Atashiriki, kuhusu Jina la movie hiyo na washiriki wengine wa movie hiyo nitayatoa maelezo hayo baadaye" alisema Twaleb. Aliendelea kwa kuongeza kuwa nia na malengo ya kampuni hiyi ni kuzitangaza filamu za kitanzania na pia kuindeleza na kuzidi kuitangaza lugha ya kiswahili ambayo tayari inazungumzwa na mataifa mbalimbali na ikisemekana kuwa moja ya lugha rahisi kujifunza. "Madhumuni ya (TE) Twaleb Entertainment ni kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu haswa kukitangaza Kiswahili katika hatua ya juu na pia kuweza kuutangaza utamaduni na desturi zetu ili ulimwengu ujue zaidi kuhusu Tanzania na lugha hii ya Kiswahili"

Pia alisema malengo ya Kampuni hiyo ni kufanya kazi Denmark na Tanzania na pia kuwatumia wasanii wengine katika kuendeleza vipaji vyao na kampuni hiyo itafanya kazi na msanii yoyote yule mwenye sifa " Nitakuwa nashirikisha wasanii mbalimbali na nitakuwa nafanya kazi hapa Denmark na pia Tanzania. Na lengo langu kubwa ni kuinua wale wenye vipaji ambao kwa njia moja au nyingine hushindwa kujiendeleza, Twaleb Entertainment ni ya wote. Soma zaidi.
Twaleb na Lucy wakiwa katika pose la picha ya pamoja
 
Filamu za kampuni hiyo zitasambazwa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania "Filamu zote zitakazokuwa zinatengenezwa na TE zitakuwa zikiuzwa katika nchi tofauti ikiwezmo Tanzania kama sehemu kubwa kiusambazaji lakini niko kwenye mipango ya kusambaza movie katika nchi yoyote ile ambayo nitakuwa na mwakilishi. Alisema pia filamu za kiswahili zinapendwa sana Denmark na soko lipo na mikakati ya filamu za kampuni hiyo ni kuinia katika soko la nchi zote jirani na Denmark yaani Norway, Germany na Sweden ambazo ni nchi zenye ushirikiano wa karibu na Tanzania.

Lucy Komba ni muigizaji wa siku nyingi ambaye licha ya kujaaliwa kipaji na kuwainua chipukizi wengi wa filamu nchini lakini kwa muda mrefu amekuwa akifanya juhudi katika kutangaza filamu za Kiswahili nchi mbalimbali na ameshatokea kwennye media kadhaa za nje ya nchi katika juhudi zake hizo kwa hiyo filamu mpya za Twaleb Entertainment na Lucy Komba sio za kukosa kwa wapenzi wa filamu za kiswahili. Pia sio mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kucheza filamu nchini kwani tayari kuna filamu ameshacheza na wasanii wengine nchini Denmark.

Twaleb and Lucy

No comments:

Post a Comment